Salim Kikeke Atambulishwa Crown FM ya Ali Kiba

 Salim Kikeke Atambulishwa Crown FM

Mtangazaji mkongwe nchini Salim Kikeke ametangazwa rasmi kuwa mwanafamilia mpya wa Crown FM.

Kupiti ukurasa wake wa Instagram, big boss wa Crown, Alikiba ameshea ujumbe wa kumkaribisha Kikeke;

My Brother @salim_kikeke hii ilikuwa ndoto na maono tuliyokuwa nayo muda mrefu. Wakati unafanya maamuzi ya kurudi Nyumbani Tanzania tulipata nafasi ya kuzungumza na nikakueleza kiu yangu yakutaka kufanya kazi na wewe Gwiji, Nguli na Mtaalam wa Tasnia hii ya Habari Afrika na Dunia.

Najua Simu zilikuwa nyingi sana lakini uliona CROWN ni sehemu sahihi sana kwako. Karibu kuwa sehemu ya Historia tunayoenda kuiandika pamoja.

Nimekuvisha Taji na CROWN Media tunaamini Hesabu zetu za Kimkakati zimekaa Sawa. Karibu sana Nyumbani @crownfmtz na @crowntvtz

Post a Comment

Previous Post Next Post