Musa Mbaroni Kwa Kumuua na Kumkata Vipande Vipande Ezenia

 

Musa Mbaroni Kwa Kumuua na Kumkata Vipande Vipande Ezenia

Jeshi la Polisi linamshikilia Abdallah Miraji maarufu kama Musa (42)mkazi wa Dar es Salaam kwa Kosa la kumuua kwa kumkata kata mpenzi wake Ezenia Stanley Kamana (36) na kisha kutupa viungo vya mwili wake maeneo mbalimbali.


Bi.Ezenia aliripotiwa kutoweka mnamo tarehe 19 Agosti, 2024 Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi na kubaini kwamba alikuwa na rafiki yake wa kiume Bw.Abdallah na ndipo akakamatwa.


Awali Mtuhumiwa amekana kumfahamu Bi.Ezenia, baada ya Viroba Vinne vyenye viungo vya mwili vikiwemo paja, vipande vya mikono, utumbo na nguo maeneo ya kunduchi,ndipo Mtuhumiwa alikiri kufanya uhalifu huo.


Mnamo Agosti 23,2024 Mtuhumiwa aliwaongoza Askari hadi eneo la Tegeta Block D na kuwaonesha alipotupa miguu na kichwa



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/bcfhIyM
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post