Ndege Aina ya ATR 72 Yaanguka Katika Makazi ya Watu na Kuwa Abiria Wote 62




Rais wa Brazil Lula da Silva ametangaza kuwa Watu wote 62 waliokuwemo kwenye ndege ya abiria iliyoanguka leo August 09,2024 huko Sao Paulo, Brazil wamefariki dunia.

Ndege hiyo iliondoka Cascavel katika Jimbo la Parana Nchini Brazil ikielekea Sao Paulo ambapo ilipoteza mawasiliano ikiwa angani na kuanguka kwenye makazi ya Watu na kisha kulipuka.

Mamlaka zimesema pamoja na kwamba Ndege hiyo ilianguka kwenye makazi ya Watu, hakuna yeyote aliyejeruhiwa au kufariki kati yao isipokuwa waliofariki ni wote waliokuwemo kwenye Ndege pekee ambapo Abiria walikua 58 na Wafanyakazi wanne.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/oPOKQCn
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post