Peter Msechu Asimulia Issue ya Kuweka Puto na Kukatwa Sehemu ya Utumbo wake




Msanii wa muziki na mdau wa lishe, Peter Msechu amesema amelazimika kukatwa utumbo ili apunguze uzito, suala ambalo amekuwa akipambana nalo kwa miaka mingi.

Hatua hiyo imekuja wakati tayari alishawekewa puto tumboni Januari 2023, ili apunguze ulaji unaomsababishia unene kupita kiasi.

Hata hivyo, amesema alipotolewa puto hilo baada ya mwaka mmoja, alirejea tabia yake ya kula kupita kiasi, hali iliyorejesha tatizo la uzito kupita kiasi.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 26, 2024 wakati akichangia mada kwenye mjadala wa Mwananchi X Space, unaoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Tanzania pamoja na Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania (TFNC), ukiwa na mada isemayo, “Je, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi ni kuimarisha afya au kujinyima uhondo?”

Msechu amesema alikutana na wataalamu wa afya waliomshauri akatwe sehemu ya utumbo, ili kupunguza ualji.

“Ikumbukwe awali nilikaa na puto mwaka mzima nikapunguza kilo 30 kutoka kilo 150 na wataalamu wakaamini nimepunguza mtindo wa kula lakini hali ikawa tofauti, kwani siku natoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kutoa puto, nilipata njaa na nilipiga simu nyumbani nikute wali maharage,” amesema.

Msechu amesema alirejea tabia yake ya kula kupita kiasi na kusababisha uzito wake kupanda tena hadi kilo 144.

“Kwa sasa baada ya kukatwa utumbo nakula kidogo sana, nimeanza kuwa vizuri huku nikishauriwa kula vizuri mbogamboga ili nipunguze mafuta na imenisaidia kupunguza kilo 27 hadi sasa,” amesema.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1MODFcv
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post