Polisi Watoa Taarifa Rasmi ya "Afande" Anaedaiwa Kuwatuma Waliombaka Binti wa Yombo

 

Polisi Watoa Taarifa Rasmi ya "Afande" Anaedaiwa Kuwatuma Waliombaka Binti wa Yombo

Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake David A. Misime, leo Agosti 24 limetoa taarifa rasmi juu ya Afisa wa Polisi Fatma Kigondo maarufu kama "Afande" anaetajwa kuhusika katika kuratibu genge la ubakaji na ulawiti kwa binti wa Yombo.


Katika Taarifa yake Jeshi la Polisi limesema kuwa Uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo umeshafanyika ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maelezo ya Fatma Kigondo na tayari jalada limekwishapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.


Taarifa hiyo ya Polisi haikueleza kiundani ni nani na nani hasa waliochukuliwa maelezo lakini nikusihi uendelee kuwa karibu na Tanzaniaweb TV ili tuweze kukujuza kila ambalo linajiri kuhusiana na kesi hiyo iliyovuta hisia za Umma wa Watanzania.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/8yGsmv6
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post