“Nilipotoka nishapasahau naangalia zaidi mbele , Feisal ni yule yule hajabadilika na nitapambana kadri ya uwezo wangu ili kuisaidia Azam”
Maneno ya Feisal Salum baada ya mechi na hata alipoulizwa kuhusu mashabiki kumzomea alijibu ni jambo la kawaida na yeye amelizoea.
Mbali na hilo nimeona huu ni mchezo wa tatu sasa kila inapokutana Azam na Yanga stori kubwa baada ya mechi huwa ni Feisal Salum
Hata vijana wanaopiga picha uwanjani huwa wanatumia muda mwingi kutafuta angle ya kupata picha ya Feisal ambayo itazungumzwa baada ya mechi kwa namna yoyote ile
Feisal anapendwa sana na mashabiki wa Yanga lakini pia uwezo wake ni mkubwa sanaa pasi na kujali anatokea wapi ni top top player, baada ya mchezo Feisal ni kawaida kupiga stori na wachezaji wa timu pinzani [ maisha baada ya dakika 90] hii chance wapigapicha wanaitumia sana kuwasaidia wazee wa zengwe
Nilitamani kumshauri aendelee kuonesha uwezo uwanjani mengine awaachie Gen-Z wa kizazi cha mtandao lakini uzuri hakuna tena haja ya kumshauri , Fei anajua kuishi na hiki kizazi ndio maana yupo pale juu hashuki zaidi zaidi anazidi kuwa bora kila siku.
Ukipata muda isikilize I miss you ya Rayvanny ft Zuchu …! msikilize tu Vanny Boy mule utanielewa na hautashangaa kwankni Feisal anazomewa sana akicheza na Yanga.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/2nWcGrU
via IFTTT