Taarifa ya ZFF inasisitiza uzushi wa kuwa uwanja wa New Amaan Complex kufungiwa hazina ukweli wowote hivyo zipuuzwe , taarifa inasema
Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) linapenda kuwatoa hofu Wadau na Wapenzi wa Mpira wa Miguu chini na kupuuza Taarifa zinazo sambazwa katika mitandao ya kijamii, kuwa Uwanja wa New AMAAN Complex haujaruhusiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutumika katika mzunguko wa Pili (2nd Preliminary Round) ya mashindano ya klabu Bingwa Afrika (CAF Interclub Competition).
Aidha ZFF, inawataarifu Umma kuwelewa kuwa, Uwanja wa New Amaan Complex umepitishwa na CAF kutumika katika mzunguko wa awali na wapili (ist and 2nd Preliminary Rounds), hivyo bado Uwanja wa New AMAAN Complex ruhusa yake ya CAF (Approval) ipo pale pale, hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya CAF ya tarehe 27 July 2024 na tarehe 26 Aug 2024.
Hivyo ZFF, inavitaka Vilabu vya dani na nje ya Zanzibar, vyenye nia ya kutaka kuutumia Uwanja wa New Amaan Complex, katika munguko huu wa Pili (2nd PreliminaryRound), kuendelea na nia yao hiyo, muhimu ni kufuata utaratibu na miongozo iliyowekwa.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/bLhs3gw
via IFTTT