Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga imebeba Ngao ya Jamii 2024 kwa ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya AzamFC kwenye Uwanja wa Mkapa katika Fainali ya Michuano hiyo, leo Agosti 11, 2024
Feisal Salum “FeiToto” ndiye aliyeanza kufunga upande wa Azam FC lakini Yanga ikasawazisha kupitia kwa Prince Dube na kuendelea kuongeza magoli mengine kupitia kwa Yoro Diaby (amejifunga), Stephane Aziz Ki na Clement Mzize
Yanga iliingia Fainali hiyo kwa kuifunga Simba goli 1-0 wakati Azam FC iliifunga Coastal Union magoli 5-2
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Jbk5Od4
via IFTTT