Abdulazak Hamza Anavyoiteka Mioyo ya Wanasimba mdogo mdogo

 

Abdulazak Hamza Anavyoiteka Mioyo ya Wanasimba mdogo mdogo

Kiwango alichokionyesha beki wa Simba, Abdulrazack Hamza katika mechi tatu dhidi ya Coastal Union (Ngao ya Jamii), Tabora United na Fountain Geti za Ligi Kuu, kimewaibua baadhi ya mastaa wa timu za Ligi Kuu kumzungumzia wakisema akiendelea kukomaa atamnyang’anya mtu namba kikosini.


Beki huyo aliyesajiliwa na Simba msimu huu kutoka Cape Town United ya Afrika Kusini, amechezeshwa katika mechi hizo kila moja akicheza dakika 90 huku akionyesha soka tamu, jambo lililompa uthubutu beki wa JKT Tanzania, Abdulrahim Seif Bausi kuamini Simba imepata mtu sahihi atakayeisaidia.


Amesema licha ya kumuona Hamza katika mechi tatu, pia aliuona uwezo wake walipocheza nayo mechi ya kirafiki waliyofungwa mabao 2-0 katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.


“Hamza ni beki mtulivu, ana uwezo wa kuona makosa yakianzia mbali na akayadhibiti. Naamini kadri muda unavyokwenda atafanya mengi katika Ligi Kuu,” alisema Bausi.


“Sina maana wazawa wanaocheza nafasi yake hawana uwezo, ila lipo jambo la kujifunza kutoka kwa Hamza ambaye hana papara pindi anapokuwa na mpira ama kuokoa hatari kutoka kwa wapinzani.” 


Mwingine aliyemzungumzia Hamza ni kiungo wa Tabora United, Abdallah Seseme aliyesema: “Simba imepata beki mtulivu na kiongozi anayeweza akatuliza presha pindi timu inapozidiwa.”


Beki huyo alisajiliwa kuchukua nafasi ya Kenendy Juma aliyekimbilia Singida Black Stars na kikosini Hamza ameshirikiana vyema na Che Fondoh Malone pamoja kuifanya Simba icheze mechi mbili za Ligi Kuu Bara bila kuruhusu bao lolote ikishinda kwa maba 3-0 dhidi ya Tabora United na mabao 4-0 ilipoumana na Fountain Gate.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/9WhncK1
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post