Dhahabu ya Shilingi Bilioni 3.4 Yakamatwa Bandarini Ikitoroshwa



Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.4 yaliyokamatwa Bandarini Jijini Dar es salaam yakitoroshwa kuelekea Zanzibar.

Baada ya kukamatwa kwa madini hayo, Waziri Mavunde leo akiongea na Vyombo vya Habari Dar es salaam, amesema Watuhumiwa hao walipofanyiwa mahojiano ya awali wamesema walikuwa wanayasafirisha kutoka bandari ya Dar es salaam kuelekea Visiwani Zanzibar na sasa uchunguzi unaendelea.

Mavunde amesema Serikali itazifuta leseni za Watuhumiwa hao pamoja na kuwaweka kwenye orodha ya Watu wasioruhusiwa kumiliki leseni ya kufanya biashara yoyote katika mnyororo wa thamani wa madini Tanzania iwapo Mahakama itawakuta na hatia.

“Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini, sasa tunapokuwa na Watu wachache ambao wanajihusisha na shughuli hizi za utoroshaji wa madini na hivyo kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia”

Akihitimisha taarifa yake, Waziri Mavunde alipongeza kazi inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya usalama na kutoa rai kwa Wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji kwani inarudisha nyuma juhudi za Serikali kukuza uchumi wa Nchi yetu


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1mSGnBU
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post