KOCHA GAMONDI AFUNGUKA: WANANCHI WANATAKA MABAO MENGI MECHI YA LEO
Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ni haki ya mashabiki wa klabu hiyo kutaka ushindi wa mabao mengi kwenye kila mchezo kutokana na namna wanavyoona ubora wa timu yao.
Gamondi amesema hayo kuelekea mchezo wa Ligi wa kesho dhidi ya KenGold ikiwa ni siku chache baada ya kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwaadhibu CBE ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili za mtoano.
“Wananchi wana haki ya kutaka mabao mengi lakini sisi ni wakweli, nimekuwa nikisema hatuwezi kushinda mabao manne au matano kila mechi, kwetu jambo la muhimu ni kucheza vizuri, kushinda michezo yetu na kuwa na mwendelezo mzuri.
“Falsafa yangu ni mpira wa kushambulia na kufunga mabao, sio tu kumiliki mpira au kupiga pasi kwangu mimi ushindi ni pale ninapoweka mpira kambani. Jambo jemba kwenye mchezo kwangu mimi na kwa mtu mwingine ni kupata bao, kama unacheza vizuri na hupati mabao basi hapo kuna tatizo, ni kama mboga kukosa sukari.
“Siangalii sana idadi ya mabao, bao 1-0 ni alama tatu hakuna kingine zaidi ya hapo, lakini yakija mabao mengi tunashukuru,” amesema Gamondi.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0yZxJtA
via IFTTT