MASTER JAY: BONGO PIA KUNA KINA DIDDY IPO SIKU WATATAJWA

MASTER JAY: BONGO PIA KUNA KINA DIDDY IPO SIKU WATATAJWA


Producer Mkongwe Master Jay amefunguka kuwa kila nchi kuna watu ambao bila wao huwezi kutoboa kwenye tasnia ya burudani, kitaalamu zaidi wanaitwa "Gatekeepers" wao wana njia zote za kukufanya ushinde tuzo, upate pesa na kazi yako ifike mbali zaidi.


Master Jay ameweka wazi kwamba hata Bongo kuna "Gatekeepers" ambao bila wao huwezi kutoboa kwenye Uigizaji au Muziki na Wasanii wa kike ndio wanapitia unyanyasaji mkubwa kwani bila kutumika kingono ni vigumu kutoboa.


Master Jay ameeleza kuwa ipo siku Wasanii wa Kike wataanza tu kutaja Wanaume wenye tabia hizo kwani ni suala la muda tu.


Sambamba na hayo amefunguka kwamba bongo hakuna Wanaume ambao wanashawishiwa kufanya mapenzi na Wanaume wenzao ili watoboe kwenye Sanaa ila kwa upande wa Wanawake wanapitia sana changamoto hii kutoka kwa Wanaume na baadhi ya Wanaume pia hupitia changamoto hii kwani hutakwa kimapenzi na Mabosi wa kike.


Master Jay amesema tatizo hilo halipo kwenye Sanaa tu bali sehemu nyingi bila rushwa ya ngono kupata kazi ni vigumu sana.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Zt8K5UL
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post