Polisi WafungukaTukio la Dereva wa Basi la Mtei Kushambuliwa Hadi Kufa..


TUKIO LA DEREVA WA BASI LA MTEI KUSHAMBULIWA HADI KUFA, POLISI YATHIBITISHA | DEREVA WA LORI AKAMATWA

Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Dereva wa lori la mizigo linalofanya safari zake nje tuhuma za kumpiga na kitu kizito dereva wa basi la Mtei na kusababisha kifo chake.

Dereva huyo amefahamika kwa jina la Gasper Roman, anashikiliwa pamoja na Utingo wake Fabris Jema raia wa Rwanda, ambao wote kwa pamoja wanadiwa kumshambulia na kumsabishia kifo Dereva wa Basi la Mtei Idd Salehe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 5, 2024 amesema tukio hilo limetokea Septemba 2, 2024.

Kamanda Makarani amesema tukio hilo limetokea kwenye eneo la Halla mjini Babati ambapo chanzo ni dereva wa lori kumshambulia dereva wa basi na kitu butu kichwani, chanzo kikiwa ni sintofahamu juu ya mgororo wa kupitana kwenye barabara baina ya madereva hao wawili wa lori na basi.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/4blVpDC
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post