SIMANZI: Kibao Akutwa Amefariki Ununio Baada ya Kutekwa Maeneo ya Tegeta

 

SIMANZI: Kibao Akutwa Amefariki Ununio Baada ya Kutekwa Maeneo ya Tegeta

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Viongozi na Wafuasi wengine wa Chama hicho pamoja na Wananchi wengine wamefika Hospitali ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala leo September 08,2024 kufuatia mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu, Ali Mohamed Kibao ambaye aliliripotiwa kutekwa juzi , kukutwa Hospitalini katika chumba cha kuhifadhia maiti ukiwa umeharibika.


Taarifa iliyotolewa leo Sept 8, 2024 kupitia ukurasa wa mtandao wa X(zamani Twitter) na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob imesema “Mwili wa Kibano ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi Ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi, kwa mujibu wa Wenyeji wa Ununio ambao ni walima mchicha, wanasema jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya kiarabu ambaye baadaye Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili Ali Mohammed Kibao ukiwa na majeraha”


Itakumbukwa jana September 7, 2024 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika aliongea na Waandishi wa Habari na kusema Kibano alikamatwa na Watu wanaodhaniwa kuwa ni Askari Polisi eneo la Tegeta baada ya gari mbili za Jeshi la Polisi kuzuia basi la Tashrif lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda kutoka Dar kwenda Tanga kisha Watu wenye silaha ikiwemo bunduki wakaondoka nae ambapo baadaye Polisi kupitia kwa Msemaji wake David Misime walisema wameiona taarifa hiyo na wameanza uchunguzi.


Kabla ya umauti wake Ali Kibao aliwahi kuwa Afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM, baadaye akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga wakati wa Rais Mstaafu Kikwete na baadaye alijiunga CHADEMA.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/CSigXc3
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post