Simba Wafanyiwa Vurugu Kubwa Baada ya Mechi Kuisha Libya, Manula Aumizwa


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kikosi cha Simba SC kipo salama Nchini Libya baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli na kisha baadaye zikaripotiwa habari kuwa wamefanyiwa vurugu.

Ahmed ameandika kwa kifupi kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kutoa maelezo zaidi ambapo ameandika “Tupo salama Wana Simba, tumefika Hotelini kwetu salama wa salmini, tujiandae sasa na mechi ya marudiano”

Kauli ya Ahmed inakuja muda mfupi baada ya Mwandishi wa Habari za Michezo wa Clouds Media, Farhan, kuandika “Simba mpaka sasa hawajafanikiwa kuondoka uwanjani taarifa kutoka vyanzo vyangu ni kuwa wanafanyiwa vurugu kubwa sana, Mashabiki wamewatupia makopo huku pia Aishi Manula amepigwa na Police akiwa jukwaani, mpaka sasa wanatazama namna ya kutoka uwanjani huku pia Refa akipigwa na Wachezaji wa Al Ahli Tripoli”


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/jJmsnpi
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post