SIMBA imetinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli Waarabu wa Libya.
Mabao manne yamefungwa ndani ya dakika 90 ambapo Al Ahli Tripoli walianza kupachika bao la uongozi dakika ya 16 kupitia kwa Cristovao Mabululu ambaye alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 kisha Simba waliweka usawa dakika ya 36 kupitia kwa Kibu Dennis na bao la pili likafungwa na Leonel Ateba dakika ya 45.
Bao la tatu kwa Simba limefungwa jioni na kiungo mshambuliaji Edwin Balua ilikuwa dakika ya 89 hivyo Simba imekata tiketi kutinga makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/gkAtN3X
via IFTTT