Wakili Godfrey Wasonga |
Godfrey Wasonga ambaye ni miongoni mwa Mawakili waliokuwa wakiwatetea kina Nyundo na wenzake ambao wamehukumiwa kifungo cha maisha Gerezani kutokana na kesi ya kumbaka na kumlawiti Binti wa Yombo, amesema wao kama Mawakili siku zote huwa wanaheshimu maamuzi ya Mahakama lakini hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.
Akiongea na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Jijini Dodoma amesema kuna mambo mbalimbali na kwamba hawakuona kama Washtakiwa hao walikuwa na kesi ya kujibu “tuliona hakuna kesi ya kujibu, huwezi kuja kuleta video za mtandao.................. kwa mfano kosa la pili hata anayeingiliwa naye alitakiwa ashtakiwe, kwanini aliruhusu wakati anasema yeye alienda kule aka-enjoy akafurahi ?” ——— Wakili Godfrey
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/d7eqkoA
via IFTTT