Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelaani vikali kitendo alichofanyiwa Mwimbaji wa Bongo Flava, Zuhura Othman Soud (@officialzuchu ) cha Mashabiki kumtupia vitu jukwani katika Tamasha la ‘Wasafi Festival’ ililofanyika Septemba 28, 2024 Mkoani Mbeya.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 1, 2024 na Kitengo cha Mawasiliano cha BASATA imeeleza kuwa Baraza hilo limetoa rai kwa Wadau wa Sanaa na Wasani kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyokua na tija na kuwataka pia Waandaaji wa matukio ya Muziki kuzingatia mazingira salama kwa Wasanii na Wadau wake katika matamasha ya Muziki.
“Baraza la Sanaa la Taifa linalaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa Mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na Mashabiki” - imeeleza taarifa hiyo.
#KitengeUpdates
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/R19HczL
via IFTTT