PSG Hawalali Wakipigania Kumsajili Mchezaji Mohamed Salah

 

PSG Hawalali Wakipigania Kumsajili Mchezaji Mohamed Salah

Kuna uwezekano mkubwa kwamba nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, ataondoka Anfield wakati wa dirisha dogo la usajili.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) inaongoza kinyang'anyiro cha kuwania kuinasa saini mchezaji huyo wa Misri.

Klabu hiyo ya mjini Paris inaripotiwa kuwa iko tayari kumpa mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya Salah kuwa mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini Ufaransa.

Mkataba wa sasa wa Salah na Liverpool unamalizika 2025, ikimaanisha kuwa anaweza kuondoka katika klabu hiyo kama mchezaji huru.

Katika siku za karibuni Salah amekuwa akihusishwa kwenda kucheza klabu za Saudia, hata hivyo mchezaji huyo anaamini sio muda sahihi kwa yeye kwenda kucheza Uarabuni.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/MvsWzVF
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post