SGR WATANGAZA KUSAFIRISHA ABIRIA 500,000 MPAKA SASA

 

SGR WATANGAZA KUSAFIRISHA ABIRIA 500,000 MPAKA SASA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema ndani ya kipindi cha miezi miwili tangu treni ya Reli ya Kisasa (SGR) ianze kufanya kazi, wamesafirisha abiria zaidi ya 500,000 ambapo hapo awali kwa kutumia Reli ya Zamani (MGR) walikuwa wakisafirisha abiria hadi 600,000 tu kwa mwaka.


Ameongeza kuwa lengo la shirika hilo ni kusafirisha zaidi mizigo na sio abiria kutokana na mizigo kuwa na mzunguko mkubwa zaidi ya watu na, kusafirisha mizigo kutawasaidia na kuwanufaisha wafanyabiashara na wameanza kwa mabehewa nane kuanza kusafirisha bidhaa mbichi ikiwemo mbogamboga na matunda.


Kadogosa amesema hayo katika stesheni ya Reli ya Zamani (MGR) ya Kilosa mkoani Morogoro, wakati wa hafla ya kuzindua mkakati wa upatikanaji wa mizigo ili kuimarisha biashara ya usafirishaji nchini kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC).



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/m9i6vSr
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post