Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Morogoro, Pwani, Visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba, Tanga na Mtwara inatarajiwa kuwa na mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.
Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imesema mvua hizo zitakazonyesha kuanzia leo Octoba 31 na Novemba Mosi mwaka huu ukanda wote wa Pwani ya bahari ya hindi zinatokana na mabadiliko ya kawaida ya hali hewa ikiwa ni katika kuelekea kuanza kwa mvua za msimu wa vuli katika maeneo yanayopata mvua kipindi kimoja kwa mwaka.
Kutokana na hilo Mamlaka hiyo imewataka wananchi walio katika maeneo tajwa na taasisi za zote za kisekta kuchukua tahadhari kuhusiana na mvua hizo.
TMA inatarajia kutoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za vuli katika baadhi ya mikoa nchini zinazotarajia kunyesha kuanzia wiki ya pili ya Novemba mwaka huu.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/vyj8xwk
via IFTTT