YANGA WAICHAPA PAMBA JIJI GOLI 4 CHAMAZI

 

YANGA WAICHAPA PAMBA JIJI GOLI 4 CHAMAZI

Mabingwa watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.


Mabao ya Yanga yamefungwa na beki Ibrahim Hamad Abdallah ‘Bacca’ dakika ya tano, viungo Mburkinabe Stephane Aziz Ki kwa penaltı dakika ya 45’+2, Mkongo Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 54 na mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 85.


Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa nne, wakati Pamba Jiji inabaki na pointi zake nne kufuatia kucheza michezo saba.


Pamba ilicheza pungufu kuanzia dakika ya 44 baada ya beki wake Saleh Abdullah kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu beki Mkongo, Chadrack Isaka Boca.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/QOok2IN
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post