BREAKING; CCM Yashinda Uchaguzi Kwa Asilimia 99.01


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mohamed Mchengerwa ametangaza matokeo ya jumla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, amesmea kuwa katika nafasi ya uenyekiti wa kijiji Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza kwa asilimia 99.01 kikifuatiwa na Chadema.

Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na 99.01%, Chadema imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79% ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na 0.09% CUF imeshinda nafasi 10 sawa na 0.08%, NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01% UMD imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01% na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01%.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/BQZbfcG
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post