'Kapteni' msaidizi wa Yanga SC, Dickson Job amewapa pole mashabiki wa timu hiyo baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo huku akiwataka wachane kalenda zenye kumbukumbu mbaya na waanze upya.
"Wananchi, poleni sana kwa Kipindi kigumu tunachopitia, Nafahamu Maumivu haya yanachagizwa na ukweli kwamba mnaipenda kwa dhati Timu yenu na Mnatuamini sana wachezaji wenu.
"Lakini Msisahau Wananchi, Hakuna wakati sisi tunakua Imara kama pale tunapopitia magumu. Nyie mnakumbuka nyakati nyingi tulizozomewa na watu wote Tulisimama tena kwa matumaini na kuishangaza Dunia ya wapenda soka.
"Wananchi, Tuchane kalenda yenye kumbukumbu zote Mbaya na tuanze upya kwa Kasi na Tamaa ya kuendelea kuwafanya Mjivunie kuwa mashabiki wa Klabu bora zaidi kwenye Taifa Letu.
"Daima Mbele, Nyuma Mwiko."
Ameandika Dickson Job kwenye ukurasa wake wa Instagram.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/r9nO2bY
via IFTTT