Jeshi la Polisi Lawakamata Watoto Wawili Kwa Kosa la Kuvunja Voo vya Treni ya SGR



Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji watuhumiwa wawili kwa kosa la kuharibu kwa kuvunja vioo viwili vya treni ya Mwendo Kasi (SGR) kwa kutumia mawe.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la polisi DCP David Misime imeeleza kuwa Tukio hilo lilitokea Novemba 22, 2024 majira ya mchana katika Kijiji cha Manase Wilaya ya Chamwino katika Jiji la Dodoma wakati Treni ya Mwendo Kasi inapita ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma.

Baada ya tukio hilo kutokea, Jeshi la Polisi lilifanya msako na kufanikiwa kuwakamata Erasto Michael Richard, Miaka 16 na Hassan Ezekiel Ndahani, Miaka 12 wote wakazi wa Kijiji cha Manase Wilaya ya Chamwino.

Chanzo cha kufanya uharibifu huo ni baada ya kuona treni ikipita wakarusha mawe kwa pamoja ili kuona kama mawe waliyorusha yataweza kushindana na mwendo wa treni.

Jeshi la Polisi limetoa wito hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ambayo treni ya kisasa inapita kuendelea kupeana elimu juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya treni hiyo kwani ipo kwa ajili ya manufaa yetu sote.

"kila mzazi/mlezi anaowajibu wa kutoa elimu kwa familia hasa watoto kuacha vitendo ambavyo vitasababisha uharibifu kwa reli na treni ya kisasa kwani itawasababisha kukinzana na sheria za nchi." - Amesema DCP David Misime


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/U0c7tbE
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post