TMA Yatabiri Mvua Kubwa Mikoa Kadhaa Kuanzia Leo



Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia leo Novemba 30 na Desemba mosi, mikoa 11 kwenye kanda tatu tofauti.

Utabiri huo, mbali na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeta, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa), umegusa ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi (Lindi na Mtwara), Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) na Kanda ya Kusini mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Morogoro.

Kwa mujibu wa utabiri huo uliotolewa Ijumaa Novemba 29, 2024, TMA imeeleza matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia Novemba 30 hadi Jumamosi hadi Desemba 3, 2024.

“Angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Nyanda za juu Kusini Magharibi mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe, Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara, Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma na Singida na Kanda ya Kusini (mkoa wa Ruvuma) na mkoa wa Morogoro,” imesema taarifa ya TMA.

Pia katika utabiri huo siku ya Desemba mosi kutakuwa na mvua kwa maeneo machache ya Nyanda za juu, Kusini Magharibi mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe, Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Utabiri huo unakuja ikiwa siku sita zimepita baada ya mamlaka hiyo kutoa tahadhari ya mvua kubwa katika mikoa minne, ikiwemo ya Nyanda za Juu Kuskazini Mashariki Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Katika utabiri huo mikoa mingine iliyotarajiwa kufikiwa na mvua hizo ni ile ya katikati ya nchi, ikiwamo Dodoma na Singida na kwa upande wa Magharibi ikiwamo Kigoma, Tabora na Katavi.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/IHdMczy
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post