Baada ya Yanga Kupata Ushindi Finyu 3 -2 Huu Ndio Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania



Young Africans siku ya leo Desemba 18, 2024 waliweza kupata ushindi finyu dhidi ya Mashujaa FC. Michuano ya Yanga SC dhidi ya Mashujaa ilichezwa katika uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam. Yanga SC leo waliingia kwa hasira, wakashambulia kweli na kipindi cha kwanza kiliisha wakiongoza kwa 2-1 dhidi ya Mashujaa FC. Magoli ya Yanga yote yaliwekwa kimiani na Prince Dube, dakika ya 8 na 21 huku la Mashujaa lilifungwa na David Uromi dakika ya 45. Kipindi cha pili, Klabu ya Yanga walikuja kwa kasi wakapata goli kupitia kwa Dude lakini Mashujaa na wakajibu kwa kuongeza moja.

Baadae Yanga wakapata ushindi wa mabao matatu kwa mawili, jambo ambalo huenda tukaliita ushindi finyu. Hadi sasa Azam FC wanaongoza na pointi 33, Simba SC 31 na Young Africans 30. Simba SC na Young Africans wamecheza mechi kumi na mbili ikilinganishwa na Azam ambao wamecheza mechi kumi na tano.



https://ift.tt/3jLDi2N

Asante kwa kusoma taarifa hii, unaweza kutoa maoni yako ili kuboresha uandishi wetu, maoni yako yatolewe kwenye nafasi ya kutoa maoni iliyopo hapo chini.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/rA0X1he
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post