Haya Ndio Mambo Kadhaa Yaliyoiangusha SIMBA Kufungwa na Waarabu

Haya Ndio Mambo Kadhaa Yaliyoiangusha SIMBA Kufungwa na Waarabu


Simba aliingia kwenye mechi na mfumo wa 3-4-3. Kwa maana ya mabeki 3 nyuma, 4 kati, na juu 3. Mfumo ulionyumbulika kwenye 4-2-3-1 wakiwa na mpira, na 5-4-1 wakiwa hawana mpira

Lengo la Fadlu lilikua kuheshimu nguvu ya mpinzani ambae yupo vizuri kwenye eneo la kati na pembeni. Fadlu alifanikiwa kipindi cha kwanza. Kivipi?

Simba ikiwa na mpira, Hamza alikua anaingia kama partner wa Okajepha kwenye eneo la chini la midfield, Ngoma alikua anasogea juu kama namba 10. Ilisaidia Simba kucheza, huku wakitafuta nafasi ya kufika mbele

Simba ikiwa haina mpira, wanakua na Flat back 5, huku ngoma akirudi kuongeza namba kwa Okajepha.

Simba ilizuia mianya yote ya mipira kupita kati, na Es Constantine alibaki na option 1 ya kupita pembeni ambako huko hakua na madhara.

Simba walikua na advantage wao wakiwa na mpira. Setup yao iliwaruhusu kucheza. Simba ilipopata mpira, kuna eneo walifeli. Je ni wapi?

Walikua na ubora kutoa mpira vizuri kwenye back-line mpaka kwenye midfield line, ila mbele hawakua na meno ya kumtafuna mwarabu

Ahoua ambae kimsingi ndiye alitakiwa kuwa driver mzuri wa mashambulizi, mipira mingi ilifia miguuni mwake. Hakua na madhara kwenye upigaji wa pasi, na mikimbio, alicheza kama mtoto katika mpira wa chandimu. Ahoua akumbushwe, anachezea Simba sio Manyema Fc.

Ateba, alikua anakaa kwenye maeneo sahihi, ila Ngoma, Kibu na Ahoua hawakua wepesi kuachia mipira kwa haraka. Ndio maana Ateba aliongoza kwa offside siku ya jana. Mikimbio sahihi, mipira ilikua inachelewa. Alioneka mzigo.

Kukosa ukomavu wa maamuzi kwenye ukuta wa Simba kuliwagharimu. Che Malone, mpira aliotakiwa ku’clear kuelekea ulipotoka, badala yake akaurudisha ndani uliwafanya wafungwe bao la pili.

Kukosa ukomavu iliwafanya Simba wasijue kipi cha kufanya hata pale ambapo walitoka kwenye mfumo wa kuzuia na kushambulia kwa kumuingiza Debora, Balua na Mukwala.

Haikua ajabu kuona Simba inamaliza mechi na Shot on target moja. Kifo cha Simba, ni kukosa meno kwenye mfumo wa Fadlu hasa timu ikiwa na mpira.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/uDVqLCH
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post