Man United Wamfunga Man City, JEURI ya Kocha Amorim Imewavusha Mashetani

Man United Wamfunga Man City, JEURI ya Kocha Amorim Imewavusha Mashetani


Mashetani hawajali umecheza mechi 11 na haujapata ushindi, wao wanaongeza chumvi pale kwenye kidonda kibichi. City kalowa.

Mashetani hawajali hauna wachezaji wako muhimu, wao kazi yao ni kukanda tu.

Sasa leo habari sio kipondo ambacho amekitoa Man United kwa City ya kipara.

Habari ni kwamba Man United imemfunga City huku Amorim akiwaacha nyumbani Rashford na Garnacho. Wachezaji hao hawakuwepo benchi, waliachwa wakiwa wazima wa afya tena kuelekea mechi muhimu na kubwa - Manchester Derby.

Ni kwamba Amorim anataka timu iwe na nidhamu iliyotukuka, isiyo na doa chafu la aina yoyote. Amorim alinukuliwa akisema leo kabla ya mechi kuwa.

“Naweka umakini kwenye kila kitu [ Kwa mchezaji ] namna anavyokula, unavyovaa kuelekea kwenye mechi, yani kila kitu. Nafanya tathmini yang halafu naamua.”

Kwa msimamo huu wa Amorim kuwatema wachezaji wake muhimu, inaonekana anataka kuitengeneza Man United iliyonyooka kama timu ya jeshi.

Mashetani kama wataweza kumvumilia kocha wao, labda wanaweza kufika nchi ya asali na maziwa.

Amorim kafanya maamuzi magumu, timu imeshinda, Mashetani yamefurahia, mwanzo mpya wenye nuru.

Kuna shabiki nyuma ya kibanda umiza huku anauliza; AMORIM AMECHELEWA. JE ALIKUA WAPI KUJA MAN UNITED MAPEMA?



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/o758Ls1
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post