Agosti 2023 rasmi alisaini mkataba wa kuingia Tanga na kuwa chini ya timu iliyopo ndani ya Mkoa wa Mahaba na mapenzi moto moto.
Aliingia Tanga akiwa kama kipa mzoefu, ambae kwa wakati huo alikua na miaka 34. Akiwa ametumikia vilabu vikubwa kama TP Mazembe, Kabuscorp Sc na Al Ansar.
Uzoefu wake ulidhihirika dhahiri kutokana na umahiri wake wa kudaka mipira na michomo mikali yenye sumu.
Akaiwezesha Coastal Union kuingia top 4 kwenye NBC PREMIER LEAGUE.
Akaiwezesha Coasta Union kufuzu CAF CONFEDERATION
Akauvunja utawala wa tuzo za kipa bora ambao ulikua chini ya Djigui Diara kwa miaka miwili, na yeye msimu wa 2023-2024 alitangazwa kama kipa bora.
Rasmi, Coastal Union wametangaza kuachana nae kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mwenyewe anasema alikua anawadai Coastal Union mishahara yake ya miezi mitatu, na walikua wanamzungusha kumlipa..
Coastal kwa upande wao wanasema, Ley Matampi alikua ana makosa mengi ambayo yameigharimu timu katika mechi za msimu huu
Kutoka kuwa kipa bora na ghafla kuvunjiwa mkataba ndani ya nusu msimu. Je kitaalamu imekaaje hii?
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/TUgRWB8
via IFTTT