Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema mauaji ya Mwenyekiti wa UVCCM, Tawi la Machinjioni Kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Michael Kalinga hayahusiani na masuala ya siasa bali yamesababishwa na biashara zake hivyo Chama hicho kimeomba Polisi wafanye uchunguzi wa kina na kutoa majibu kuhusu suala hilo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani ameiambia @AyoTV_ kuwa Chama cha CCM kimegharamia jeneza, chakula na taratibu zote za mazishi hayo ambayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
“Alipigiwa simu kwenda kufuatilia kitoweo kwasababu yeye ni Mfanyabiashara anajihusisha na majiko ya kuchoma nyama, wakati anaenda kuangalia kitoweo akiwa na mwenzake akapata changamoto hiyo na umauti ulimkuta, wale waliomuua wakamchukua mwenzake na kumpeleka barabarani wakamuacha” - Ngonyani.
“Tumeona mitandaoni Watu wanaongea vitu ambavyo hawavijui, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kuchunguza, tukio hili lisihushishwe na jambo lolote linalohusu siasa, sisi kama Mkoa wa Mbeya hatujawahi kuwa na kashikashi za namna hiyo kisiasa, tukio hili linahusishwa zaidi na shughuli za utafutaji kwenye kazi zake za utafutaji, Watu wasioongee wasiyoyajua na kutengeneza taharuki mitandaoni, kama huwezi kuelezea tukio hili ni bora ukae kimya” - Ngonyani
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/rDm7A9l
via IFTTT