Anaandika ✍️
@cheyolutenganotz
Ukisema kukosa namba kwa Chama Yanga kunatokana na umri wake kwenda nitakataa, kwa sababu kuna mastar kibao wenye umri sawa na yeye na bado wanakiwasha tu,
Kama ni amekutana na wachezaji bora kuliko yeye inaweza kuwa sababu lakini kwangu ni amekosa imani tu yule bado ni mchezaji hatari kumbuka bado ni National team material na anacheza.
Nakumbuka wakati Saido yupo Yanga mara yake ya kwanza kuja Tanzania alikuwa na umri zaidi ya Chama lakini kumbukumbu zangu zinasema alihusika kwenye mabao 17 katika michezo 18 aliyowatumikia wananchi mabao 10 pasi 7 za magoli.
Aliondoka Yanga kwa tatizo la kinidhamu baada ya kutoroka kambini yeye na Dickson Ambundo,
Unajua Saido alifanyaje? .....
Yule mtaalamu aliamini bado anauwezo wa kukiwasha vizuri tu tena pale pale Kariakoo,
Alitafuta njia akaenda kwa wachimba madini Geita gold akacheza pale kwa kipindi kifupi tu akitumikia michezo 10 ambayo ilimtosha kufunga mabao manne lakini akihusika kutengeneza magoli 6,
Desemba 29 wakati wa dirisha la usajili limefunguliwa Simba wakamchukua hapo mtego wake ukakamilika akajiunga unyamani akitokea Geita.
Msimu wake wa kwanza tu alichukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi akipacha na Fiston Mayele,
Jamaa alifunga magoli 13 na pasi za magoli 6 kwenye mechi 12 imagine huu ulikuwa kati ya usajili ulio ingia moja kwa moja bila maswali
Ukisema ligi alibahatisha mrejee kimataifa akiwa na Simba kipindi kile Simba ikifunga magoli 9 yeye alihusika kwenye magoli manne 4 pasi za magoli 2 lakini akifunga yeye mara 2
Zingatia umri wake lakini alienda Geita Gold timu ndogo akazalisha magoli na pasi, alicheza Simba yenye kina Jobe, Fredy na akawa mchezaji tegemezi.
Leo tunakumbuka nyakati zake bora Tanzania akicheza mechi 67 kwa kipindi kifupi lakini akihusika kwenye magoli 53
Age is just a number,
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Famhl0I
via IFTTT