“Mko tayari kwa uchaguzi...Niwaombe muda utakapofika mkiunge mkono Chama cha Mapinduzi na kumetolewa taarifa, ya vyama vya siasa kusaini makubaliano ya kanuni za uchaguzi, vyama vyote mnavyovijua vimesaini makubaliano hayo maana yake ndivyo vitakavyoshiriki uchaguzi."
“Kwa bahati mbaya, lakini siyo kwa bahati mbaya, ni watu ambao waliamua mwaka huu wapumzike, hao waliokuja hapa walikuwa wamechoka sana, mwaka huu wameamua kupumzika na mimi niliwaambia hawa hawajajiandaa na uchaguzi, hawa wana migogoro na leo imethibitika, hawajaenda kusaini, maana yake hawatashiriki uchaguzi,”
“Chama chako hakitakuwepo, wewe kapigie kura Chama Cha Mapinduzi, kwa hiyo leo ni rasmi kwamba jamaa wamekataa kusaini lakini tuliwatabiria kwamba hawajajiandaa na wanaonekana kuchoka na mtu aliyechoka hutakiwi kumlazimisha aendelee na safari. Mtu anakwambia goti linauma, mtu anakwambia pumzi inakata, hivi utaendelea kumwambia twende?”
“Kwa hiyo, wenzetu wale wamethibitisha leo kwamba hawatakuwa sehemu ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu na hata ikitokea uchaguzi mdogo hawatashiriki kwa miaka mitano,”
"Zile mbilinge mbilinge na vichekesho walivyofanya hapa zote ni kazi bure, kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba ndiyo timu ambayo imekimbia mechi aah, hawa walishachoka, hawawezi muziki wa Chama Cha Mapinduzi.
“Wao leo wamepoteana na wamethibitika kwa hiyo tutakuwa na vyama vingine lakini hao wengine waliokuja juzi hapa hawapo tena. Na mimi nitoe rai kwa wanachama wa chama hicho kwa sababu hawatashiriki uchaguzi basi wana uhuru wa kupiga kura,” amesema Katibu wa Itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Ndugu Amos Makalla wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi katika Uwanja wa Maulid ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/bN2MOz7
via IFTTT