Akiwa Liwale Mkoani Lindi leo Aprili 11,akiambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Amos Makalla, Mch. Peter Saimon Msigwa ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi ni Chama kinachojali na kuzingatia maslahi ya wananchi, kikijitofautisha kabisa na vyama vingine vilivyopo nchini Tanzania.
Wakati wa Mkutano wa hadhara, Mch. Msigwa ameeleza kuwa siasa zinazohusu uchumi na ustawi wa watu ndizo zinazoshuhudiwa ndani ya CCM, akieleza kuwa alipokuwa Chadema walielekezwa kupinga kila jambo, suala ambalo lilimfanya kuwa kipofu na kutoona kazi nzuri zinazofanywa na serikali katika kuhudumia wananchi.
" Kule nilipokuwa chochote cha Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kupinga tu, serikali ikisema inajenga bwawa la Mwalimu Nyerere tunapinga, Nchi ikiwa gizani tunalalamika.Serikali ikisema inanunua ndege, shirika la ndege limekufa tunapinga halafu kwenye ndege hizo hizo tunapanda na Kombati zao.Hawa ni watu pingapinga na pingapinga sio sera, CCM inajulikana kwa kile inachokisimamia." Amesema Mch. Msigwa.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/OKt7XFW
via IFTTT