Tarehe 9 Mnyama Anatakiwa Kufunga Goli Tatu Bila, Ateba Anatakiwa Kukimbia Kama Kichaa

Tarehe 9 Mnyama Anatakiwa Kufunga Goli Tatu Bila, Ateba Anatakiwa Kukimbia Kama Kichaa



Kama tarehe 9 Fadlu ataendelea kumuamini Ateba,basi inabidi amtete kwa mashabiki wa Simba.

Tarehe 9 Simba wanatakiwa kupanda mlima wa Everest,Mnyama anatakiwa kufunga goli 3 dhidi ya timu ngumu kuruhusu na hatari kwenye Counter Al Masry,wakati huo wanatakiwa kuzuia kama watumwa.

Takwimu zinaonyesha mechi ya kwanza Simba walitawala mchezo huku wakipiga jumla ya mashuti 18 na 7 yakilenga lango ila Simba hawakuwa na nafasi kubwa (BIG CHANCE) hata moja….hivyo Siyo rahisi kuwafungua Masry na wala hutarajii kupata nafasi 20 kwenye huo mchezo.

Kaka Ateba ukipata nafasi ya kuanza basi siku hiyo unatakiwa kuacha utoto,muda wote unatakiwa kukimbia kama kichaa ili kutafuta mashimo,na siku hiyo unatakiwa kubadilisha nusu nafasi na nafasi kamili kuwa magoli unless utaiangamiza Simba na utabeba lawama kubwa.

Binafsi natamani kuona Mukwala akianza kwani ndo mshambuliaji mwenye form na confidence ya kufunga kwa siku za hivi karibuni,lakini pia Mukwala ni “opportunist” ambaye anajua muda wakuwa nje na ndani ya box.

Kazi kwako Kaka Ateba,maana nchi Yangu na mashabiki wake nawaju.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/yFizfK8
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post